Mrisho Mpoto - Adela

Copied!edit Lyrics
original text at lyrnow.com/1993757
Inro
Nyosha kidole, Adela
Sina nia mbaya ya kukurudisha darasani
Nyosha kidole, Adela
Sina nia mbaya ya kukurudisha darasani

Verse 1
Adela, nyosha kidole
Sina maana nataka kukurudisha darasani, la!
Nataka nijue uwepo wako kama yu hai
Ili maneno yangu nisiyatupe
Siku zote kuni ya akiba huicheka inayoungua jikoni
La moyoni huponzwa na ulimi
Asiyeona nafsi yake haoni akionyweshwa (haoni, ye-ey)
Wewe ndio shuhuda na mwanga wa kweli
Maana kila anaetoka huko anatingisha kichwa
Toka kushoto kwenda kulia
Toka kulia kwenda kushoto
Anakataa hatujui, anasikitika hatuelewi
Inakuwa ngumu kujua mdogo wangu (inakuwa ngumu)
Sasa hivi maisha kila kitu kimekuwa dili
Kila anayerudi anakitambaa mkononi, tena kimeloa (kimeloa)
Cha ajabu, vyote vya rangi moja
Walijiandaa kulia? Mimi sijui Adela
Liishalo ndio dogo kuliko linalokuja
Isije kuwa hadithi ya ndovu aliyeponzwa na pembe zake
Labda kwa kuwa ni msimu wa joto, ndio maana walikuja navyo

Chorus
Nyosha kidole, Adela
Sina nia mbaya ya kukurudisha darasani

Verse 2
Adela ule mshindo niliousikia sio mdogo
Wala sijawahi kuusikia kabla
Zaidi ya shuleni, tеna kwenye mfano wa
Kitabu cha mwalimu Nyika
Aliniambia, "Ukisia, fyu!
Ujue ndеge za kivita wanajeshi wanajiandaa na siku ya mashujaa
Ukisikia kengele na adhana
Watu wanakumbushwa kufanya ibada kumrudia Mungu wao
Lakini ukisika, boom! Ujue ni bomu"
Je, ndivyo ilivyo huko?
Nyoosha kidole nikwambie kilichokuwa moyoni mwangu
Siunajua kuwa bahari haivukwi kwa kuogelea
Na ukitaka kufuga ng'ombe lazima uanze na kuku?
Hakuna jinsi maisha lazima yaendelee
(maisha lazima yaendelee)
Adela mwambie mjomba kuwa
Chiriku mzee akamatwi kwa makapi
Ni wajanja tu hao, dalili ya ushehe sio kilemba
Ni heri kujikwaa kidole kuliko ulimi
Mwambie si kila anaempigia makofi anamshangilia
Wengine ni wanafiki na wazandiki wakubwa
Wanapiga kumtaka amalize kuongea
Na ili kuwajua asikilize mlio wa makofi wanayompigia, atagundua
Kama hana muda kwa sababu ya majukumu ya hapa na pale
Basi ayarekodi asikilize taratibu akiwa afisini kwake (oh, Adela)
Usipokuwa makini mdogo wangu utayumbishwa
Mwambie mjomba kuwa kuregarega sio kufa
Kufa ni kuoza utumbo
Watakuja tu, kuhani na kuomboleza msiba
Kwa lugha rahisi wanakuja kuanua matanga
Mwambie hujafa
Wengine watakuja na vipande vya nguru mkononi
Si wanajua unanjaa
Sawa, unanjaa na kweli upo tayari kumla nguru huyo
Lakini waulize kaoshwa? Kama hajaoshwa usile!
Nitakwambia kwanini
Harufu yake itakuchukia karne nzima kuisha
Roho za watu kufanya chumba cha mtihani
Au mtaji wa kwenda ukingoni mwa bahari, ni makosa
(ni makosa)

Chorus
Nyosha (nyosha) kidole Adela (oh, Adela)
Sina nia mbaya ya kukurudisha darasani (ye-iye, mama)

Verse 3
Tumekuwa mitaji sasa
Mwambie halipendezi machoni, hata mbele ya Mungu
Ni kweli, matazizo hayana mahali pengine pa kutokea
Isipokuwa Duniani
Lakini kwa nini kila siku ni sisi tu?
Anaekueleza ya wengine, chunga mdomo wako
Hatashindwa kuwaeleza wengine yakwako
Neno ningejua huja mwisho wa safari
Sio kosha lako Adela, ni mjomba ndie hataki kuisikia sauti yangu
Eti, sina jipya, sikufanya vizuri shuleni, ripoti yangu haikumfurahisha
Amesahau kuwa ticket yake ya safari nimemkumbusha mimi
Alipoisahau mchagoni
Hebu waangalie na wale, hali mbaya sana kwa akina Adela
"Idadi inatisha, wamekufa kinyama"
"Haijawai kutokea Duniani"
Hivyi ni vichwa vya Habari tu
Katika baadhi ya vyombo vyetu vya habari hapa nchini
Hivi sisi tukisema hivyo; Dafur, Iraq, Sudan, Afghanistan
Wao waripoti vipi vyombo vyao vya habari?
Msije mkaleta siasa kwenye roho za watu
Tutashindwa kuwaelewa
Mjomba, chura anapenda maji, lakini sio ya moto (mjomba)
Kuvua kina kirefi kunataka uzoefu (kunataka uzoefu)
Tunasafari ndefu sana, lakini maisha lazima yaendelee

Chorus
Nyosha kidole (nyosha) Adela (oh, Adela)
Sina nia mbaya ya kukurudisha darasani (bororo, iye mama)
Nyosha kidole (nyosha dada) Adela (oh, dada)
Sina nia mbaya ya kukurudisha darasani darasani
Nyosha kidole Adela (kidole)
Sina nia mbaya ya kukurudisha darasani (darasani)
Nyosha kidole Adela (ooh)
Sina nia mbaya ya kukurudisha darasani (darasani, darasani)
 
0

Song Description:

edit soundcloud

SoundCloud:

edit soundcloud

More Mrisho Mpoto lyrics

Mrisho Mpoto - Adela
{Inro} Nyosha kidole, Adela Sina nia mbaya ya kukurudisha darasani Nyosha kidole, Adela Sina nia mbaya ya kukurudisha darasani {Verse 1} Adela,